Header

Stamina akutwa akirecord Wasafi Rec na kuzungumzia kukamilika kwa Album yake na Roma kama ROSTAM

Rapa kutoka Tanznaia na mkali wa michano anayewakilisha mkoa wa Morogoro, ‘Stamina’ amefunguka kuhusu kuithamini nafasi ya kufanya kazi na lebo ya muziki ya WCB Wasafi  katika kolabo ya Remix ya wimbo ‘Mpe Habari’ wa rapa Stereo aliyomshirikisha Rich Mavoko.

Akipiga Stori na Dizzim Online Stamina amesema kuwa moja ya kitu ambacho anaamini kimemeuongezea heshima kutokana na uwepo na thamani ya muziki wake katika kiwanda cha muziki wa Tanzania ni kufanikisha tukio hilo la kufanya kazi katika lebo hiyo kubwa ya Wasafi kupitia ushiriki wake katika Remix ya ‘Mpe Habari’ ambayo inategemewa kushirikisha wakati kibao kutoka Tanzania na Khaligraph kutoka Kenya..

Hata hivyo Stamina ameongeza taarifa za kuwa yeye na rapa Roma wamesha kamilisha album ambayo imememshirikisha muimbaji Ben Pol kama ROSTAM, muunganiko unaowakutanisha katika kuwapatia mashabi ladha ya aina mbili tofauti za muziki wao.

Msikilize Stamina katika Exclusive na X-KiPande ya Dizzim Online.

Comments

comments

You may also like ...