Header

Usain Bolt ashindwa kutimiza ndoto yake kucheza Manchester United

Mshindi mara nane wa Medali ya Dhahabu katika Mashindano ya Olimpiki Usain Bolt amethibitisha kuukosa Mchezo wa Heshima kati ya Manchester United dhidi ya Barcelona unaohusisha Wachezaji wa zamani wa Vilabu hivyo kutokana na kuendelea kusumbuliwa na Majeraha.

Bolt, 30 alipata tatizo la misuli ya paja wakati akishiriki mashindano ya Riadha ya Dunia maarufu kama World Athletics Championships katika mbio za mita 4x100m yaliyofanyika nchini London yakiwa ni Mashindano yake ya Mwisho kushiriki baada ya kutangaza kustaafu.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter Bolt ameweka picha inayoonyesha Picha ya Jeraha lake ambalo litamfanya akae nje kwa Miezi mitatu huku akikosa Mechi hiyo ambayo inatarajiwa kupigwa Septemba 2 katika Dimba la Old Trafford.

Bolt alijumuishwa katika kikosi cha United ambacho kilikuwa na nyota wengine wa zamani wa Klabu hiyo wakiwemo Edwin van der Sar, Paul Scholes, Denis Irwin, Dwight Yorke, Phil Neville, Ronny Johnsen, Louis Saha, Mikael Silvestre, Jesper Blomqvist, Quinton Fortune pamoja na Dion Dublin ambacho kitacheza na kikosi cha Wachezaji wa zamani wa Barcelona ambao wameshastaafu kucheza soka wakiongozwa na Erick Abidal

Comments

comments

You may also like ...