Header

Vanessa Mdee na Maua Sama kuja na wimbo wa pamoja

Vanessa Mdee na Maua Sama wanatarajia kuja na wimbo wao pamoja hivi karibuni. Taarifa hiyo imetolewa na Vanessa wakati akihojiwa kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa hii.

Muimbaji huyo amesema Maua ni mwanamuziki anayemkubali sana na hivyo kurekodi naye ngoma ni kitu ambacho alikuwa akikifikiria kwa muda. Vee amesema wimbo huo umefanyika katika studio ya BK Records chini ya producer aitwaye Breezy Baby.

Kwa sasa Vanessa anafanya vizuri na wimbo wake Kisela aliomshirikisha Mr P wa kundi la P-Square huku Maua akiwa na wimbo mpya uitwao Katukatu.

Comments

comments

You may also like ...