Header

Maua Sama: Ukichanganya muziki na mapenzi lazima ufeli

Maua Sama amechat na Dizzim Online kuhusu madhara ya msanii kuchanganya mapenzi na muziki kwa wakati mmoja.

“Yaani kiukweli kabisa bila kupindisha ukiendekeza mapenzi na kazi lazima upande wa kazi utaAthirika kwa kiasi kikubwa sana,” amesema Maua. “Tufahamu kila kitu kina sehemu yake na kila kitu kina nafasi yake, tukiwa kazini tufanye kazi na kwa upande wangu siwezi kuendekeza mapenzi hata siku moja,” ameongeza.

Kwa upande mwingine Maua Sama amewaomba mashabiki waipe shavu ngoma yake mpya Katukatu aliyoitoa hivi karibuni.

Comments

comments

You may also like ...