Header

Mo Music azungumzia kolabo alizofanya nje ya nchi na kubadili mfumo wa kuachia nyimbo

Staa kutoka katika kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva Tanznaia ‘Moshi Katemi’ a.k.a Mo Music anayefanya vyema na ngoma yake ‘Usiniache’ aliyomshirikisha Barakah The Prince, amezungumzia ngoma alizojipanga nazo kwa lengo la mfululizo wa kuziachia moja baada ya nyingine katika hatua za kubadilisha mfumo wake wa kukaa kimya kwa muda na kuchelewa kuachia ngoma.

Akipiga stori na Dizzim Online Mo amesema kuwa ni kweli mfumo wa kazi zake umekuwa hautabiriki kwa maana kuachia nyimbo kipindi ambacho kinaacha muda mrefu kiasi cha mashabiki kusubiria sana ambapo sasa amewahakikishia mashabiki kuwa baada ya kuachia hii kolabo yake mpya atachia kazi kwa mfumo wa kutoacha nafasi kubwa ya mashabiki kusubiria na kuzungumzia ngoma alizofanya na wasanii wa ndani na nje ya Tanzania.

Msikilize Mo Music katika mahojiano na Dizzim Online.

Comments

comments

You may also like ...