Header

Alikiba alijibu dongo la Diamond kwenye Fresh Remix

Uhasama kati ya Diamond na Alikiba umepamba moto wiki hii. Ni baada ya Diamond kumpiga vijembe hitmaker huyo wa Aje kwenye remix ya wimbo wa Fid Q, Fresh. Maishari ya rap ya Chibudenga kwenye wimbo huo yanasema:

Kunicompare na Cinderella haiwezi kuwa fresh/ Simba kutoka mbuga ya Tandale/
Naona swala wanaforce tuwe sare sare/ Viuno vidogo wanataka pensi ya Pepe Kalle/
Si walitaka kiti, nimewapa hadi kitanda wakalale

Hatimaye Kiba ametumia Twitter kujibu diss hiyo:

Kiba ameandika: I know that you hate me 100% but I give ZERO F**ks 🤙🏾 #KingKiba

Kwenye remix hiyo ya Fresh Ray Vanny pia ameshirikishwa.

Comments

comments

You may also like ...