Header

Mark Wahlberg ampiku The Rock kama muigizaji anayelipwa fedha nyingi zaidi

Mandatory Credit: Photo by Andrew H. Walker/REX/Shutterstock (7728567i) Mark Wahlberg The National Board of Review Awards Gala, Arrivals, New York, USA - 04 Jan 2017

Staa wa filamu ya “Transformers: The Last Knight”, Mark Wahlberg amempiku Dwayne Johnson aka The Rock na kuwa muigizaji wa Hollywood anayelipwa fedha nyingi zaidi kwa kuingiza dola milioni 68 mwaka jana kwa mujibu wa jarida la Forbes.

Muigizaji huyo ambaye zamani alikuwa rapper ajulikanaye kwa jina la Marky Mark, amemzidi staa wa “Baywatch” Johnson aliyeingiza dola milioni 65, huku muigizaji mwenzake wa “The Fate of the Furious” Vin Diesel akiingiza dola milioni 54.5.

Wengine ni Adam Sandler aliyekamata nafasi ya nne kwa kuingiza dola milioni 50.5 na Jackie Chan akikamata ya tano kwa kuingiza dola milioni 49.

Comments

comments

You may also like ...