Header

England yatangaza kikosi, Nathaniel Chalobah na Harry Maguire wajumuishwa.

Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya England West Southgate ametanga kikosi cha Wachezaji 23 kitakachocheza Michezo ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia mwezi Septemba dhidi ya  Malta na Slovakia.

Katika Kikosi hicho ambacho Nahodha wa wao wa zamani Wayne Rooney hajajumuishwa baada ya kutangaza kustaafu siku ya Jana kimeongeza majina mapya wakiwemo Harry Maguire pamoja na Nathaniel Chalobah ambao wamejumuishwa kwenye kikosi hicho kwa mara ya kwanza.

Kikosi hicho cha Wachezaji 23 kilichotajwa ni:

Joe Hart (West Ham United, Jack Butland (Stoke City), Jordan Pickford (Everton), Tom Heaton (Burnley), Ryan Bertrand (Southampton), Aaron Cresswell (West Ham United), Gary Cahill (Chelsea), Phil Jones (Manchester United), Harry Maguire (Leicester City), John Stones (Manchester City), Michael Keane (Everton), Chris Smalling (Manchester United), Kyle Walker (Manchester City), Kieran Trippier (Tottenham Hotspur), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Nathaniel Chalobah (Watford), Jake Livermore (West Bromwich Albion), Jordan Henderson (Liverpool), Raheem Sterling (Manchester City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Marcus Rashford (Manchester United), Danny Welbeck (Arsenal), Jesse Lingard (Manchester United), Dele Alli (Tottenham Hotspur), Harry Kane (Tottenham Hotspur), Jamie Vardy (Leicester City), Jermain Defoe (AFC Bournemouth), Daniel Sturridge (Liverpool).

England ambao ni vinara kundi F wakiwa na jumla ya alama 14 itacheza Michezo hiyo Septemba 1 dhidi ya Malta ambao wanashika Mkia katika Kundi hilo wakiwa hawana alama yoyote huku ikimalizia dhidi ya Slovakia Septemba 4 wenye alama 12.

   Makundi ya Kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2018.

Comments

comments

You may also like ...