Header

Mshindi kati ya Mayweather dhidi ya McGregor kuondoka na “Money Belt’

Halmashauri ya Mchezo wa ngumi Duniani kupitia kwa Rais wake Mauricio Sulaiman wametangaza Mkanda ambao utagombaniawa na Mabondia Floyd Mayweather dhidi ya Conor McGregor kwenye Pambano lao litakalofanyika Agosti 26 Mjini Las Vegas nchini Marekani.

Mkanda huo ambao unafahamika kwa jina la Money Belt umetengenezwa na madini mbalimbali ikiwemo Dhahabu na utakabidhiwa kwa Mshindi wa Pambano hilo Licha ya kiasi ambacho kila Bondia atakabidhiwa ambacho ni zaidi ya dola za kimarekani Milioni 100. Thamani ya Mkanda huo ni zaidi ya ule wa pambano kati ya Mayweather dhidi ya Manny Pacquiao.

Mayweather ambaye anashuka kwenye Pambano hilo baada ya kutangaza kustaafu Mchezo huo  wa ngumi atakutana na Bingwa wa UFC Conor McGregor pambano ambalo linasubiriwa sana na Wapenzi wengi wa Boxing Duniani.

Comments

comments

You may also like ...