Header

Baada ya kumaliza adhabu yake, Gareth Bale arejeshwa timu ya Taifa ya Wales

Baada ya kumaliza adhabu yake ya kufungiwa Mchezo mmoja Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale amerejea katika kikosi cha timu ya Taifa ya Wales kinachojiandaa na Michezo ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018.

Bale, 28 amekosa Mchezo dhidi ya Serbia wa kundi D mwezi Julai baada ya kupata kadi mbili za njano kwenye Mchezo dhidi ya Jamuhuri ya Ireland. Kocha mkuu wa Wales Chris Coleman amemjumuisha kwenye kikosi nyota huyo ambae ameisaidia timu yake ya Real Madrid kunyakua Ubingwa wa Uefa Champions League Mara mbili mfululizo.

Joe Ledley ambae ni Mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na timu ya Crystal Palace amejumuishwa pia katika kikosi hicho cha wales kitakachocheza Mwezi Septemba dhidi ya Austria na Moldova.

Kikosi kamili cha Wales: Wayne Hennessey, Danny Ward, Adam Davies, Ben Davies, James Chester, Neil Taylor, Chris Gunter, Jazz Richards, James Collins, Tom Lockyer, Ashley Williams, Ethan Ampadu, Joe Allen, David Edwards, Andy King, Lee Evans, Joe Ledley, Aaron Ramsey, Jonathan Williams, Gareth Bale, Marley Watkins, Hal Robson-Kanu, Sam Vokes, Tom Lawrence, Ben Woodburn.

Wales wapo Kundi D nafasi ya tatu wakiwa na jumla ya alama 8 nyuma ya Vinara wa kundi hilo Serbia wenye alama 12 pamoja na Jamuhuri ya Ireland wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na alama 12 pia.

Comments

comments

You may also like ...