Header

Jux afunguka kuhusu ngoma ya ‘Utaniua’ kuyazungumzia mahusiano yake na Vanessa Mdee

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania Juma Mussa Mkambala a.k.a Jux ameyazungumzia mahusiano yake na muimbaji Vanessa Mdee na kwa namna ambayo wimbo wake mpya wa ‘Utaniua’ katika wazo la mahusinao  yake na kupatikana kwa wazo zima la wimbo.

Akizungumza na Chilly na Sky ya Dizzim Online, Jux amesema kuwa ingawa maandalizi ya kufanya wimbo huo kupitia mdundo uliotumika katika wimbo yalikuwepo lakini kukamilika kwa wazo la wimbo umezungumzia zaidi hali ya kimapenzi na kuachana kwake na mpenzi wake wa zamani muimbaji Vanessa Mdee.

“Sasa hivi ni miezi mitano tangu tume-break up, …kitu ambacho nimekiimba kwenye ile nyimbo ni kitu ambacho nilikuwa katika ile hali ya hivyo, kitu ambacho nimekiongea nimekitoa moyoni kwangu yaani ni nyimbo ambayo nimeiimba kutoka moyoni na mtu aliyesababisha kuimba kwenye ile nyimbo ni Vanessa” Amesema Jux.

Msikilize Jux katika mahojiano na Dizzim Online.

Tazama video ya wimbo mpya ‘Utaniua’ wa Jux.

Comments

comments

You may also like ...