Header

Golikipa Simba kuelekea India kwaajili ya matibabu ya Goti

Golikipa wa Klabu ya soka ya Simba Said Mohamed Nduda amepata matatizo ya goti ambayo yatamfanya kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya Majuma Manne huku akitrarajia kuondoka nchini wiki hii kuelekea India kwaajili ya Matibabu.

Nduda aliumia mazoezini wakati Wekundu hao wa Msimbazi wakijiandaa na mchezo dhidi ya Yanga wiki iliyopita, Matibabu hayo yatamuweka mchezaji huyo nnje kati ya wiki nne hadi sita kabla ya kujiunga tena na wenzake kwa ajili ya mazoezi na anatarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa wiki hii.

Aidha wachezaji John Bocco na Haruna Niyonzima ambao walipata Majeraha madogo tayari wamereja kikosini na wameshaanza mazoezi na wenzao hii leo.

Comments

comments

You may also like ...