Header

Jackline Wolper avuka maji kula bata na Mpenzi wake Mpya

Staa wa kike wa filamu kutoka Tanzania Jackline Wolper wikendi iliyopita amelitafuna bata nje ya Tanzania akiwa na mpenzi wake mpya ambaye amechukua kitu cha aliyekuwa penzi wake Staa wa ngoma ya ‘Sina’ Harmonize.

Kupitia ukurasa rasmi wa mpenzi mpya wa Wolper na Brown zilipostiwa picha za wawili hao wakiwa uwanja wa ndege picha ambazo ziliambatana na maelezo ya kimahaba mahaba na kutoa ishara ya kuwa ni safari ya kuvuka maji na kwenda zao Zanzibar kwa kutumia usafiri wa ndege.

Hata hivyo baada ya picha za kuonesha kuwa ni safari ya Zanzibar ya Couple hiyo mpya mjini kupitia akunti zao wote wawili zilituma picha ambazo wazi wazi ziliwaonesha katika pozi za kufurahia maisha ya bata za hapa na pale huku mbali na picha kusema yote yanayohusu mahaba ya wawili hao  pia waliongeza msisitizo kwa jumbe kwenye picha hizo.

🏊‍♀️🏊‍♂️I love Zanzibar @official_brown_ #mine

A post shared by Jacqueline Wolper (@wolperstylish) on

Solved ❤ @official_brown_

A post shared by Jacqueline Wolper (@wolperstylish) on

Vile vile penzi hili linaonekana wazi kuwa ni tiba ya kidonda kilichoukuta moyo wa Jackline Wolper kwa kipindi cha mwisho wa mahusiano yake na Harmonize na pia kuwa Brown amekuwa chaguo pekee kutoka kwa wote waliohitaji kuwa naye kimapenzi kwakuwa Wolper alishaiambia Dizzim Online kuwa amekuwa akipokea maombi mengi sana ya wanaume wakiomba kuwa naye kimapenzi.

Comments

comments

You may also like ...