Header

Mark Zuckerberg na mkewe Priscilla Chan wapata mtoto wao wa Pili

Mkurugezi mtendaji na mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg na mkewe Priscilla Chan wamepata mtoto wao wa pili aliyepewa jina la August Chan Zuckerberg ‘Agosti’.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook, Mkurugenzi Mtendaji huyo aliweka ujumbe/barua ndefu ya furaha yao kwa kumkaribisha mtoto wao ‘August’ pia wasiache kukumbushia iliyokuwa furaha pia walipomkaribisha kifungua mimba wao Maxima Chan Zuckerberg ambaye ni dada wa mtoto wao huyo.

Mtoto wao huyo wa pili  haijulikani kama sababu za kupewa jina ‘August’ ni kwakuwa amezaliwa mwezi huu wa Nane/Agosti lakini kwa wengi wao inahisiwa hivyo ambapo bado Zuckerberg na Chan ambao wametimiza idadi ya watoto wawili wa kike inabaki ikikumbukwa kuwa walipata mtoto wao wa kwanza binti Maxima, mwezi Novemba, 2015.

Posted by Mark Zuckerberg on Monday, August 28, 2017

Comments

comments

You may also like ...