Header

Amber Lulu na Young D sio poa, Kisa ni picha za nusu utupu

Msanii  wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania anayefanya vizuri na ngoma yake ‘Watakoma’ Amber Lulu na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani rapa Young D wameingia kwenye vuta ni kuvute kisha kikiwa ni picha ambazo ziliwaonesha wakiwa ni wenye kupakwa mafuta na kusambaa isifahamike imeibukia wapi ambapo Young D amedai kuwa picha hiyo zmevuja tu kwa bahati mbaya.

Muda mfupi baada ya kusambaa kwa kasi kwa picha hizo, Young D alipaza sauti kupitia ukurasa wake wa Instagram kujieleza ambapo kwa mujibu wa maneno yake alionekana kuwa amesikitishwa na kusambaa kwa picha hiyo ambayo ilimuonesha kuwa katika vazi la sketi ‘Scottish’ isieleweke nini maana ya mtoko huo ambapo mbali na kudai kuwa ilivuja bahati ambayi bado aliongeza kuwa picha hiyo ni kati ya picha zilizopigwa katika behind The Scene bila kueleza katika tukio lipi.

Muda mfupi baadae Amber Lulu naye hakusita kujieleza kuhusu picha hiyo ambapo kwa mujibu wa maelezo yaliyoambatana kwenye picha aliyoweka kupitia akaunti yake ya Instagram, Amber amesema kuwa lawama za kuwa yeye ndiye aliyevujisha picha hiyo sio kweli na ni picha za kipindi cha nyuma katika wimbo wa ‘Bongo Bahati Mbaya(BBM)’ wa Young D.

Comments

comments

You may also like ...