Header

Wanawake kuchukuliana mabwana sio poa – Jacqueline Wolper

Msanii kutoka kiwanda cha filamu nchini Tanzania, Jacqueline Wolper amezungumzia tabia ya mastaa wa kike kuchukuliana wanaume.

“Ukweli sio vizuri,” Wolper ameiambia Dizzim Online.

“Japokuwa mapenzi ni kitu cha ajabu sana na mimi ilishawahi kunitokea. Kuna bwana wa bongo movie mwenzangu aliwahi kunitaka kipindi hicho hata mapenzi siyajui vizuri, so nikamuona mtu wa ajabu sana. Kumbe kwenye mapenzi huwezi kujudge  hasa kama umepitia vikwazo vingi na unayajua mengi kwenye mapenzi, yaani eti huyu aliwahi kuwa na nani wala alifanya nini kwenye mapenzi,” ameeleza.

Aidha mrembo huyo aliongeza, “pia sisi wasanii tunazunguka sehemu ile ile tunakutana sehemu zile zile tumekuwa tukionana wale wale so mwisho wa siku ndo inapelekea kuwa hiyo.”

Wolper kwa sasa yupo kwenye mahusiano na mwanaume anayefahamika kwa jina la Brown.

Comments

comments

You may also like ...