Header

All Star na Jay Moe kupamba ligi ya kikapu Dar

Wadhamini wakuu wa ligi ya kikapu ya RBA, kampuni ya StarMedia Tanzania Limited imeandaa mechi ya All Star ambayo itashirikisha wachezaji vinara katika ligi hiyo inayotarajiwa kuchezwa siku ya Jumamosi Septemba 2 mwezi wa tisa.

Baada ya kuanza kwa hatua ya robo fainali (playoffs), wapenzi wa mpira wa kikapu Tanzania Kwa ujumla watapata nafasi ya kushuhudia wachezaji vinara wa ligi hiyo. Mchezo utahusisha timu mbili ambazo zimepewa majina ya NYOTA na MAMBO, majina ambayo ni ya vifurushi vya gharama vya StarTimes Mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Ndani wa Taifa majira ya saa saa 2 hadi saa 4 Usiku.

Mchezo huo wa All Star ni ishara ya kuanza kwa hatua ya Mtoano (PlayOffs) ambayo itahusisha jumla ya timu nane (8), ili kumpata mshindi na timu tatu (3) zitakazopata nafasi ya kushiriki ligi ya Taifa hapo baadaye mwaka huu. Hatua hiyo inatarajiwa kuanza tarehe 6 Septemba.

Licha ya Mchezo huo wa All Star burudani ya Muziki kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Juma Mchopanga maarufu kama Jay Moe atatumbuiza pia ili kunogesha Mechi hiyo pamoja na Ligi hiyo.

Comments

comments

You may also like ...