Header

Jux amualika kwa hisia Vanessa Mdee katika sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake

Staa wa ngoma ya ‘Utaniua’ kutoka kwenye kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva, Juma Jux ameendelea kutumia maneno yanayotuma ujumbe kwa mhusika na mashabiki kuwa anaukumbuka sana na kuutamani uwepo wa aliyekuwa mpenzi wake muimbaji Vanessa Mdee ambaye waliachana miezi kadhaa iliyopita.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Jux alituma ujumbe akizungumzia enzi za furaha yake kipindi ambacho hakuwa na usherehekeo mkubwa sana akikumbuka sherehe ya mwisho kubwa aliyoshiriki 2013 huku akimtaja Vanessa kuwa ndiye mtu aliyekuwa akimpa faraja zaidi kwa vipindi vyote ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwake.

Katika kusherekea siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake mwaka huu Jux amewaalika mashabiki wake huku asiache kumuomba Vanessa japo aje siku hiyo na kuelezea kuwa faraja kubwa taipata kama atamuona tarehe 1 Septemba katika ukumbi wa Hyatt Regency ulioko jijini Dar Es Salaam.

Ujumbe huu kutoka kwa Jux ambao unaonesha kuwa ni wazi kabisa anamkubuka na kuukosa kwa dhati uwepo wa Vanessa unaunganika katika mazungumzo ya Jux na Dizzim Online kuwa wimbo wake mkpya ‘Utaniua’ ulitungwa kwa wazo la hisia za upendo kwa Vanessa.

Yasikilize na kuyatazama mahojiano kati ya Dizzim Online na Juma Jux.

Comments

comments

You may also like ...