Header

Naj adai amezipa mgongo filamu kwa sasa

Najma amesema kwa sasa focus yake ni kwenye muziki na sio filamu.

Naj ambaye hivi karibuni aliachia ngoma yake, Utanielewa, ameiambia Dizzim Online kuwa kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja inahitaji akili ya ziada ingawa bado anapenda kufanya zote.

“Niseme kwamba nafanya vitu vyote ingawa ni ngumu kuigiza na muziki  ila for now nimejikita zaidi kwenye muziki. Lakini hivi karibuni nilishawahi kufanya tamthilia na kina JB na nina uhakika kwa mashabiki zangu wa upande wa uigizaji watakuwa washaisikia,” amesema.

“Lakini ki ukweli kazi zote napenda kuzifanya  ila kwa sasa wataniona sana kwenye muziki na nikipata kwenye movie nitafanya tena,” amesisitiza.

Miongoni mwa filamu alizowahi kufanya ni Fan’s Death akiwa na Ray Kigosi.

Comments

comments

You may also like ...