Header

Shamsa Ford: Mume wangu hawezi kuoa mke wa pili

Msanii wa maigizo nchini Tanzania, Shamsa Ford amesema mume wake Chid Mapenzi hawezi kuoa mke wa pili hata kama dini yake inaruhusu.

Akipiga story na Dizzim Online muigizaji huyo amesema mume wake hawezi kufanya kitu kama hicho kwasababu hakuna anachokosa kwake.

“Mume wangu kuoa mke wa pili haiwezekani yaani hawezi  kwasababu hana sababu ya kufanya hivyo,” amesema. “Mimi namridhisha kwa kila kitu.  halafu pia mimi mwenyewe nilishawahi kumgusia suala la mke wa pili kwasababu dini yetu inaruhusu, akasema hawezi kwasababu mke wa pili tutaanza kukaribisha mambo ya ushirikina, umaskini na kutokuendelea kimaisha,” amesisitiza.

“Na kama ikija kutokea ndo anataka kuoa  mke wa pili  nataka anipe sababu za kujitosheleza  na ziwe za msingi.”

Shamsa ni mke wa mfanyabiashara huyo ambapo bado hawajabahatika kupata mtoto pamoja.

Comments

comments

You may also like ...