Header

Video mpya ya Taylor Swift yapata views milioni 43 Youtube ndani ya siku 1

Video mpya ya Taylor Swift imeweka rekodi ya Youtube kwa kutazamwa mara milioni 43.2 ndani ya siku moja. Video ya wimbo huo uitwao “Look What You Made Me Do” imeivunja rekodi ya wimbo wa Psy, Gentleman iliyopata views milioni 36 katika saa 24 mwaka 2013.

Swift pia amevunja rekodi ya saa 24 ya Vevo iliyokuwa ikishikiliwa na video Adele ya mwaka 2015, Hello iliyopata views milioni 27.7 katika siku yake ya kwanza.

Comments

comments

You may also like ...