Header

Wizkid kupakua kolabo yake na rapa Future

Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria Wizkid ameendeleza ubabe katika kuachia kolabo kubwa zote alizofanya kipindi ambacho amekuwa akitajwa kuwa msanii anayefanya vizuri katika muziki wake hasa mwanzoni mwa mwaka 2015, 2016 na mwaka huu wa 2017.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Wizkid amewataarifu mashabiki wa muziki wake kuwa siku ya leo ataachia kazi ambayo ni kolabo na Staa wa kimarekani rapa ‘Future’ ikiwa ni ngoma ya kolabo kubwa baada ya ile aliyofanya na rapa na muimbaji mkanada Drake ‘Come Closer’, ‘Gbese’ aliyomshirikisha Trey Songz na nyinginezo...

Hata hivyo Wizkid ni kati ya wakali ambao wanafanya vizuri kiasi cha kukubalika sana na mastaa wa muziki wanaofanya vizuri kimataifa ambao hata wengine ashafanya nao kazi kama vile Trey Songz, Diplo, Chris Brown na wengine huku ikibaki kama historia katika muziki wake anaweza kutajwa kuwa ni msanii wa kutoka Afrika amabye amefanikisha kolabo nyingi na mastaa wa kimataifa ndani ya muda mfupi.

Comments

comments

You may also like ...