Header

50 Cent aikiponda kituo kinachoonesha series yake ya Power, aisifu BET

Pamoja na mafanikio makubwa ambayo series yake ya Power imeyapata mwaka huu, 50 Cent hana furaha na kituo kinachoionesha, Starz.

Rapper huyo anaonekana kupunguza morali wa kufanya kazi na kituo hicho, huku nguvu yake kubwa sasa akielekeza kwenye kituo cha runinga cha BET ambako huko ameanzisha show yake iitwayo 50 Central itakayoanza kuruka mwishoni mwa mwezi ujao.

Fif ametumia Instagram kurusha dongo kwa Starz na kuimwagia sifa BET.

“Im starting to think BET is better then STARZ. I don’t want to kiss nobody over there. Now @ConnieOrlando interim head of programming of BET😘All day. LOL #50centralbet,” ameandika.

50 Central itaanza kuoneshwa kupitia BET Septemba 27.

Comments

comments

You may also like ...