Header

‘Full Dozi Concert’ kuwasha moto viwanja vya Dar Live ‘Septemba 9’

Katika kuhakikisha wapenda Burudani ya muziki wanapata burudani ya wasanii wanaowapenda kupitia muziki wao tarehe 9 ya mwezi Sepetemba jiji zima litahamia viwanja vya Dar Live Mbagala kushuhudia tamasha la Full Dozi Concert.

Tamasha hilo lililopewa nguvu ya kutosha na ITV, Redio One na Capital litawadondosha wakali wa burudani ambao ni pamoja na Juma ‘Kassim’ Nature, Snura, Beka Flavour, Q Chief(Q-Chillah), Sholomwamba, Twanga Peteta na wakali wengine ambao wataongezwa katika orodha ili kunogesha burudani ya usiku huo.

Mapema katika uzinduzi na kutangazwa rasmi kwa Tamsha hilo, Q Chief na wengine walihaidi kufanya makubwa jukwaani kwakuwa mbali na kuwa atalitumia jukwaa na wasanii wakali wapya, yeye pamoja na wakongwe wenzake watahakikisha wanakata kiu ya mashabiki wa muziki kwani sio kawaida kwao kutoa burudani chini ya kiwango.

Comments

comments

You may also like ...