Header

Madonna ahamia Ureno ili kumsaidia mwanae wa kuasili David Banda atimize ndoto zake za soka

Staa wa pop wa nchini Marekani, Madonna amelazimika kuhamia mjini Lisbon, Ureno ili mwanae wa kuasili, David Band mwenye miaka 11 ajiunge na academy ya soka ya Benfica. Jarida la kila wiki la Visao limeandika, “Madonna si mtali tu, anaishi Lisbon.”

Madonna amekuwa akikaa kwenye hoteli huko Lisbon baada ya kununua nyumba katika kijiji kiitwacho Sintra, kilichopo kilomita 30 kutoka mji mkuu wa Ureno. Alinunua nyumba hiyo kwa dola milioni 9.

David Banda, aliyeasiliwa na Madonna kutoka Malawi mwaka 2006, amejiunga na kituo cha mafunzo cha Benfica katika kitongoji cha Seixal. Banda ni mmoja wa watoto wanne ambao Madonna aliwaasili kutoka Malawi wakiwemo mapacha aliowachukua mwezi wa pili. Ana watoto wawili wa kuwazaa mwenyewe.

Comments

comments

You may also like ...