Header

Harry kane hajaupenda mwezi wa mwisho wa majira ya usajili

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya England pamoja na klabu ya soka ya Tottenham hotspurs Harry Kane amekiri kutoupenda mwezi wa nane ambao dirisha la usajili linafungwa barani Ulaya baada ya kuonyesha kiwango kidogo katika mechi za mwanzo wa ligi kuu.

Kane,24 ambaye hajafunga goli Mwezi Agosti, usiku wa jana Septemba 2 amefunga magoli mawili katika ushindi wa mabao manne  wakati timu yake ya Taifa ikicheza mchezo wa kufuzu kombe la Dunia 2018 dhidi ya Malta.

kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter Kane ameweka picha akiwa katika Mchezo huo na kuandika maneno ambayo yanasomeka “sijaupenda mwezi wa nane kwakweli! Timu imeonyesha kiwango kizuri na matokeo mazuri kwenye uwanja wa ugenini”.

 

Comments

comments

You may also like ...