Header

UEFA yaanza uchunguzi kwa klabu ya PSG juu ya matumizi ya Fedha

Shirikisho la soka Barani Ulaya UEFA limeanza uchunguzi katika klabu ya Paris St German hususani katika kukagua uvunjwaji wa sheria mpya ya Shirikisho hilo ya Klabu kutumia fedha nyingi kuliko kiasi inachoingiza ili kupata mafanikio inayofahamika kama ‘UEFA Financial Fair Play Regulation’ FFP.

Hatua hiyo ya Shirikisho inakuja baada ya PSG kufanya usajili ghali duniani wa Mchezaji Neymar Jr. kutoka Barcelona kwa ada ya Paundi milioni 220 ada ambayo imeongezeka paundi milioni 100 zaidi ya ile ya Mchezaji ghali msimu 2016-2017 kiungo Paul Pogba huku timu hiyo ikihusishwa pia kutoa zaidi ya Paundi Milioni 160 kwa kinda Kylian Mbappe ambaye amejiunga na Klabu hiyo kwa mkopo akitokea Monaco.

Sheria hii ya Financhial Fair Play ilianzishwa mwaka 2010 ikiwa na lengo la kuzuia Vilabu mbalimbali Barani Ulaya kutotumia Pesa nyingi katika kuliko zile Klabu inazoingiza ili kuepusha kufirisika au kushindwa kuendesha klabu kwa muda mrefu huku adhabu ya kufungiwa kusajili au kupigwa faini ikitolewa kwa Klabu itakayokutwa na kosa hilo.

Klabu ya PSG ambayo imeshinda mara Sita ubingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa inamilikiwa na kampuni ya Gulf state of Qatar ya mjini Doha huko Qatar chini ya Rais Nasser bin Ghanim Al-Khelaïfi.

 

Comments

comments

You may also like ...