Header

Lil Wayne ashambuliwa na kifafa tena, akutwa amepoteza fahamu hotelini

Rapper wa Marekani, Lil Wayne Jumapili amekutwa katika chumba cha hoteli aliyokuwa amefikia akiwa hajitambui. Kwa mujibu wa TMZ, Weezy alipatwa na kifafa. Staa huyo alikimbizwa katika hospitali ya Northwestern Memorial ambako alidaiwa kushambuliwa tena na kifafa.

Wayne alikuwa anatarajiwa kutumbuiza na kundi la Rae Sremmurd kwenye kiota cha Drais Beachclub huko Las Vegas baadaye jioni, lakini madaktari walimshauri abaki hospitali. Wawakilishi wa Wayne wameiambia TMZ kuwa show ya Wayne iliahirishwa ili apumzike.

Hii si mara ya kwanza Wayne kupata kifafa. Amekuwa akipata matatizo hayo kwa muda ikiwemo mwaka 2012 ambapo ilibidi ndege aliyokuwa anasafiria kwenda Los Angeles itue kwa dharura Texas baada ya kupata kifafa.

Comments

comments

You may also like ...