Header

Maria Sharapova atupwa nje US Open

Mwanadada Maria Sharapova ambaye ni Mcheza Tenisi ametupwa nje katika mashindano ya US Open baada ya kupoteza mchezo raundi ya nne dhidi ya Anastasija Sevastova.

Sevastova, 27 ambaye alitangaza kustaafu mwaka 2013 kabla ya kurejea tena katika Tenisi mwaka 2015 ameshinda kwa jumla ya seti 5-7 6-4 6-2 dhidi ya Sharapova na kutinga hatua ya robo fainali ambayo atakutana na Mmarekani Julia Goerges katika hatua hiyo.

Sharapova, 30 ambaye anashika nafasi ya 146 kwa ubora kwa upande wa Wanawake alirejea tena uwanjani mwezi April mwaka huu 2017 baada ya kumaliza adhabu yake ya kufungiwa kutokana na kutumia madawa ya kuongeza nguvu Mchezoni kwa muda wa zaidi ya miezi 13.

Comments

comments

You may also like ...