Header

Mastaa wawili wa muziki Duniani wafariki ndani ya wikendi moja

Misiba miwili imeiangukia tasnia ya muziki wa Country Duniani ambapo siku ya Ijumaa ya wiki hii amefariki muimbaji mashuhuri kutoka Marekani ambapo imethibitika kuwa mwanamuziki Troy Gentry amefariki katika ajali ya helikopta iliyotokea mida ya saa saba mchana huko Medford, New Jersey.

Troy Gentry

Akiwa ni mwenye umri wa miaka 50 mauti yakamkuta, Troy ajali iliyopelekea kifo chake  imetokea mapema Ijuma siku ambayo jioni ya siku hiyo alitengemewa kuwa tatumbuiza mijini  Medford.

Msiba mwingine, Jumamosi ya tarehe 9 mwezi Septemba mashabiki na wapenzi wa muziki wa Country wamepokea tena taarifa nyingine za kumpoteza Staa wa muziki huo ‘Don Williams’ ambaye amefariki ghafla akiwa ni mwenye umri wa miaka 78.

Don Williams

Don ambaye ni mzaliwa wa Portland, Texas amefariki ghafla kwa kuugua ndani ya muda mfupi ambapo taarifa za kufariki kwake zimethibitishwa na afisa wake wa mawasiliano.

Comments

comments

You may also like ...