Header

Vanessa Mdee ana collabo na staa wa dancehall wa Ghana, Stone Bwoy

Vanessa Mdee amesema anakuja collabo na msanii wa Ghana na mshindi wa tuzo ya BET, Stone Bwoy. Ametoa taarifa hiyo kwenye mahojiano na Ayo TV wakati wa Fiesta ya Arusha.

Stone ni mmoja wa wanamuziki wa dancehall wanaokubalika zaidi Afrika.

Mwaka 2017 Vanessa Mdee amefanya collabos na wasanii wengine wakubwa wa Afrika. Pamoja na kumshirikisha Peter Okoye wa P-Square kwenye Kisela, ameshirikishwa na wasanii kama Reekado Banks na Orezi wa Nigeria pamoja na Tay Grin wa Malawi.

Wiki iliyopita pia Vee alishoot video hapa Dar ya wimbo alioshirikishwa na msanii wa Zambia, Roberto. Mwaka huu Vee Money ataachia album yake, Money Mondays.

Comments

comments

You may also like ...