Header

Uvumi mpya wa mahaba mapya wanukia kwa Diamond Platnumz na Staa wa Namibia

hb c Mjasiriamali, Muigizaji na Mshindi wa Big Brother Africa msimu wa nane mwaka 2013 wa nchini Namibia Dillish Mathews na Staa wa muziki wa Bongo Fleva Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz wameingia kwenye kuzungumziwa zaidi katika mitandao ya kijamii kupitia tetesi za kuwa kuna dalili za kuota kwa mimea ya mahusano ya kimapenzi kati yao.

Dillish Mathews

Kufuatia milolongo wa matukio ya picha za Dillish Mathews na Diamond Platnumz kuonekana kuwa inafanana katika sura ya kulandana kwa matukio zimeibuka rasha rasha za uvumi kuwa wawili hao hivi karibuni walitembelea Zanzibar kwa lengo la mapumziko huku ikitajwa hotel iliyoko ukanda wa bahari ya Hindi ya Diamonds La Gemma dell’Est kuwa ilitumika kwa mapumziko.

Muonekano wa sehemu ya kuvinjali katika Hotel ya Diamonds La Gemma dell’Est nyakati za usiku

Eneo la ufukwe la Hotel ya Diamonds La Gemma dell’Est

Kingine kilichowafanya baadhi kuongeza umakini katika kufatilia hiki kinachoendelea kusemekana, ni post iliyosambaa mitandaoni ikionesha kuwa moja ya akaunti ya Dillish alipost picha yenye maneno ya utata wa maneno na herufi za majina ambayo baadhi waliyatafsiri kuwa ni ufupisho wa jina lake Dillish mwenyewe na Diamond “Bae is Working. DND”.

Post ya Dillish Mathews iliyozua utata

Hili likiwa zima zima bado ni tetesi, chumba cha habari kinalifanyia kazi kujua muelekeo wa taarifa hizi ili kubaini ukweli ambao utaweka wazi uhai au kifo cha penzi la Zarinah Hassan ‘Zari’ na Diamond Platnumz.

 

 

Comments

comments

You may also like ...