Header

Beyonce, Nicki Minaj, Drake na wengi wachanga $44m kusaidia wahanga wa mafuriko Houston

Kampeni ya “Hand in Hand: A Benefit for Hurricane Relief” iliyohusisha nyota wa Marekani wakiwemo Beyoncé, Drake, na Nicki Minaj, imekusanya takriban dola milioni 44 kusaidia waathirika wa mafuriko jijini Houston.

Mastaa wengine walioshiriki ni pamoja na Justin Timberlake, Diddy, Cassie, Gwen Stefani, Jamie Foxx, Selena Gomez, Will Smith, Questlove, Oprah Winfrey, na Vic Mensa.

Hadi kampeni hiyo inamalizika zaidi ya dola milioni 44 zilichangwa ikiwemo dola milioni 5 toka kwa Apple.

Tukio hilo la saa moja liliondaliwa na Bun B na Scooter Braun.

Comments

comments

You may also like ...