Header

Dk Mwakyembe: Nimenukuliwa vibaya, sijafuta shindano la Miss Tanzania

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo amekanusha taarifa ya jana kuwa amepiga marufuku mashindano ya Miss Tanzania kutokana na kuendeshwa kwa ubabaishaji mkubwa.

Alisema amenukuliwa vibaya kwenye mahojiano na Times FM. Dk Mwakyembe amesema alichomaanisha ni kuwa serikali itawapa vibali watu kuendesha mashindano hayo iwapo tu watahakikisha kuwa zawadi wanazoahidi wanazionesha kwanza na pia kuhakikisha muendelezo wake.

Baraza la Sanaa la Taifa limetoa taarifa ya ufafanuzi wake:

Kwenye mahojiano na Times FM, Mwakyembe alisema:

“Tulikuwa na Miss Tanzania hapa, mimi nimepiga marufuku. Hatuwezi kuwa tuna waparade watoto wetu, wanafanya kazi hii wakitegemea utapata gari, anatafuta hilo gari mwaka mzima, sasa huo ni uswahili ambao mimi siwezi kuukubali nikiwa kiongozi wa hii wizara. Kwahiyo nimewakatalia wote, hakuna cha Miss Tanzania. Nataka ukitaka kuanzisha hilo shindano, nataka uniwekee hilo gari uniwekee pale ofisini uniachie na switch, zawadi ya pili ni pikipiki sita basi ziwe pale nawaambia bwana ruksa,” ameongeza.

Dk Mwakyembe alisema serikali itakutana na watu wanaoeleweka kuandaa mashindano hayo kwa uhakika wa kuwepo muendelezo na utoaji zawadi usiokuwa na chenga chenga.

“Hata tuzo za muziki, zilikuwa zinategemea baadhi ya watu, wakinuna basi hiyo tuzo haipo, hatuwezi kwenda namna hiyo,” aliongeza.

Comments

comments

You may also like ...