Header

StarTimes yaendeleza vipaji na kukuza kiswahili Tanzania

Kampuni ya huduma za Matangazo ya kidigitali StarTimes imeendeleza nia yake ya kuibua vipaji kwa wenye uwezo na nia katika tasnia ya uigizaji Tanzania kwa msimu wa pili mfululizo wa shindano la maigizo ya sauti.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja Mahusiano wa kampuni hiyo Ndg. Juma Suluhu amesema kuwa lengo la shindano hilo ni kukuza matumizi ya lugha ya Kiswahili na kuwapatia fursa vijana wa kitanzania kuonyesha vipaji vya sauti katika tasnia ya maigizo na kujitengenezea mazingira mazuri ya ajira.

“Mwaka huu tumefanya mabadiliko makubwa katika Shindano hili, kubwa la kwanza ikiwa ni kuongezeka kwa Mkoa mwingine ambao utafikiwa na Shindano hili. Mwaka jana tulifanya Zanzibar, Dar es Salaam na Arusha lakini mwaka huu tutafika hadi Mwanza” Amesema Juma Suluhu.

Shindalo hilo lililopewa maudhui ya lugha ya Kiswahili lililofanyika katika kumbi za hoteli ya Colosseum limeudhuliwa wadau mbalimbali ambao ni pamoja na viongozi wa BAKITA na wahadhiri wa somo la Kiswahili kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Hata hivyo Shindano hili kutokana na mafanikio makubwa ya msimu uliopita imewasukuma kuyawekea muendelezo ambapo mara hii Usaili wa kwanza wa shindano la  pili katika msimu huu mpya utafanyika visiwani Zanzibar Jumamosi hii tarehe 30 Septemba na baadaye tarehe 8 Oktoba, Usaili utahamia Mwanza kabla ya kurejea Dar es Salaam tarehe 14 Oktoba. Kwa wakazi wa mikoa ya jirani.

 

 

Comments

comments

You may also like ...