Header

Swizz Beatz na Fabolous wawapa ‘shout out’ Diamond na Mwana FA

Bongo Flava to the world, thanks kwa jitihada za Flaviana Matata na connection zake Marekani. Jumanne hii producer wa Marekani, Swizz Beatz alikuwa akifanya uzinduzi wa nguo zake, Bally x Swizz na Flavy alikuwa mmoja wa wageni waalikwa.

Kwenye hafla hiyo alifanikiwa kukutana na Swizz ambaye alirekodi selfie akiwasalimia watanzania na kumtaja Diamond Platnumz. Diamond aliipost pia video hiyo na kuandika: Doh! You guys make me want to fly to America now!😃…. see you on the 8th Oct, poppin @officialbelaire champagne day and night!! @therealswizzz @flavianamatata.

Pia Flavy alirekodi selfie nyingine akiwa na rapper Fabolous ambaye alimpa shout out Mwana FA.

Naye FA amepost video hiyo na kuandika: All my friends know how i ‘understand’ Loso..@flavianamatata done made my year,not a day not a week not a month,A YEAR aisee..thanks for the S/O @myfabolouslife i have always been a big fan! NB;Sjui kama ntawaruhusu kunywa hata maji siku mbili hizi,i cant promise 😜

Kwenye uzinduzi huo pia Kisela ya Vanessa Mdee na Seduce Me ya Alikiba zilichezwa.

Comments

comments

You may also like ...