Header

Diamond Platnumz na kundi la Morgan Heritage wakata kiu ya mashabiki kwa wimbo huu ‘Hallelujah’

Kundi la muziki wa rege lenye chimbuko la Jamaika linaloundwa na watoto watano wa msanii maarufu wa rege Denroy Morgan ‘Morgan Heritage’ na Staa wa muziki wa Bongo Fleva ‘Diamond Platnumz’ wamekunjua mkeka wa ngoma yao ya pamoja inayokwenda kwa jina ‘Hallelujah’ chini ya utayarishaji wa Laizer Classic na Studio za Wasafi Record.

Diamond Platnumz katika kuinogesha kazi hii mpya amesikika katika uandishi wa lugha ya Kiswahili lakini zaidi akiimba kwa matumizi ya lugha ya kiingereza na inaweza kukubalika kuwa ameendana sana na mdundo wa ngoma hii katika mianguko ya maadhi ya dancehall hivi huku akichanganya na miguso ya melody ya RnB kwa kuchop moja ya kionjo kutoka katika wimbo wa Joe Thomas ‘I Wanna Know’.

Video imeonekana kuwa inaweza kumteka mtu katika ubusy wa kuburudishwa na kinachoonekana ni imesheheni warembo wenye mionekano ya haina yake chini ya uongozwaji wa Director mkubwa wa video za muziki mzaliwa wa Nigeria na kukulia London Mr. Moe Musa.

Comments

comments

You may also like ...