Header

Dele Alli afungiwa Mechi moja na kupigwa Faini

Kiungo wa timu ya Taifa ya England pamoja na Klabu ya Soka ya Tottenham Hotspurs Dele Alli amefungiwa Mechi moja na ya timu ya Taifa pamoja na kupigwa Faini baada ya ishara ya ishara ya kidole cha kati aliyoonyesha katika Mchezo dhidi ya Slovakia.

Alli, 21 ataukosa Mchezo wa Alhamisi dhidi ya Slovania pamoja na kulipa faini ya Paundi 3,852 baada ya Shirikisho la soka Duniani FIFA kushindwa kukubaliana na kauli ya dele Alli kuwa alikua anamuonyesha ishara hiyo Mchezaji mwenzie Kyle Walker kwenye Mchezo huo ambao England iliibuka na ushindi wa 2-1.

Tukio hilo lilitokea katika Mchezo dhidi ya Slovakia dakika ya 77 baada ya Dele Alli kugongana na Beki Martin Skrtel wakati wachezaji hao wakiwania Mpira huku Mwamuzi wa Mchezo huo Clement Turpin akiamuru Mpira uendelee na kuwa hakuna Madhambi yoyote yaliyofanyika ndipo Dele akaonyesha ishara hiyo.

Comments

comments

You may also like ...