Header

Diamond Platnumz avunja rekodi ya Ali Kiba kwa masaa

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz ambaye wengi wao wamesikika zaidi wakimuita Chibudenga kutokana na a.k.a yake nyingine ya CHIBU , bila shaka wengi wenu mmeshasikia jina hilo. Usiku wa saa tano tarehe 28 mwezi Septemba mwaka huu Diamond Platnumz aliachia video ya wimbo wa kolabo yake na kundi la wakongwe wa muziki wa rege kutoka Jamaika ‘Morgan Heritage’ inayokwenda kwa jina ‘Hallelujah’ ngoma ambayo imevunja rekodi ya nyimbo zilizowahi kufanya vizuri mtandao ukanda wa Afrika Mashariki.

Rekodi ya video ya muziki kutazamwa zaidi ndani ya muda mfupi kutoka Tanzania ilishikiliwa na Staa wa ngoma ya ‘Aje’ Ali Kiba kupitia wimbo wake wa ‘Seduce Me’ ulioingia katika rekodi ya watazamaji zaidi ya milioni moja ndani ya muda wa masaa 38 huku ikishikilia nafasi ya kwanza kati ya video zilizokuwa katika trend ya video za muziki zinazofanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube.

Ndani ya muda masaa 15 video ya ‘Hallelujah’ amevunja rekodi ya kupata watazamaji zaidi ya milioni moja kwenye mtandao wa YouTube huku ikiendelea kuwa katika nafasi ya kwanza ya video zinzofanya vizuri kwenye mtandao huo(#1. Trending) sambamba na asilimia kubwa ya maoni kutoka kwa wadau na mashabiki yenye ishara za wazi wazi kuwa muziki wa Tanzania umeingia katika ramani nzuri ya kulitangaza taifa la Tanzania kimataifa zaidi.

 

Comments

comments

You may also like ...