Header

Diamond Platnumz, Wikipedia na mitandao mingine hakuna mwenye kosa katika hili??

Staa wa muziki wa Bongo Fleva kutoka Tanzania Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz ni staa ambaye kila mwaka anasherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwake tarehe 2 mwezi October kwakuwa ni tahere ambayo Bi. Sandra alimkaribisha mwane wa kiume Duniani kwa uchungu kisha ikafuata furaha ya kuitwa mama Naseeb.

Lakini kwa mashabiki wenye kumfatilia Staa huyu mara kadhaa wamekuwa wakikutana na kumbukumbu ya kuzaliwa kwake katika sherehe tarehe tofauti kabla ya tarehe husika ambayo ni tarehe 2 Octoba. Mwaka 2014 Diamond Platnumz alifanya sherehe kubwa katika maudhui ya kuadhimisha siku yake hiyo tarehe 25 kitu ambacho ilitofautiana katika tarehe lakini maudhui yakiwa ni yale yale.

Maana kubwa inawezekana tarehe husika isitumike katika kusherehekea kwakuwa inaangukia/dondokea katika siku ambayo inaweza kuwa na changamoto ya waalikwa na wahusika wote wasiweze kushiriki kulingana na ratiba zao za kimajukumu au isiwe siku nzuri sana kwa lengo la kusherehekea hasa kiabishara zaidi kwakuwa kwa mtu maarufu kila haina ya mkusanyiko wa jambo fulani nafasi hiyo ina asilimia kubwa ya kutumika kibiashara zaidi.

Kingine sababu ya kutofautiana kwa tarehe katika kusherehekea inaweza kuwa ni majukumu ya kibiashara pia katika sura ya kuwa mhusika(Diamond Platnumz) anaweza kuwa katika ratiba nyingine ya kibiashara ambayo itambana kushiriki moja kwa moja katika siku husika hivyo inaweza kuwa ni sababu ya kupelekea msherehekeo katika siku tofauti na siku lengwa lakini ni ndani ya maudhui tu ya kumbukumbu ya mfanano wa siku ya kuzaliwa.

Taarifa sahihi za mtandao wa kutunza kumbukumbu za kuzaliwa kwa mastaa na watu mashahuri Duniani (Diamond Platnumz)

Mwaka huu imeonekana kabisa kuwa Diamond Platnumz anamaandalizi makubwa ya kusherehekea siku ya mfanano wa kuzaliwa kwake na ni kwasababu tu ya dalili za maandalizi ya mwaka huu. Picha linaanza na kuwandaa wote wenye shahuku ya kusherehekea naye kwakuwa tayari ametangaza kuwa tarehe 29 ya Mwezi Sepetemba ni siku ya party la kwanza kuelekea siku husika ya Birthday yake itakayofanyika katika ukumbi wa Element jijini Dar es Salaam chini ya udhamini mkuu wa kinywaji cha mvinyo cha Luc Belaire akiwa ni balozi wa kinywaji hicho Afrika.

Ikitazamiwa kuwa mashabiki wa Diamond Platnumz wanangoja kwa hamu ujumbe au chochote kitakachosemwa/kuandikwa katika mtandao na mapenziwe Zari The BossLady, kuna kila dalili za kuwa kusherehekea kwa Diamond Platnumz na mashabiki zake kwa udhamini mkuu wa Luc Belaire mashabiki wategemee kuwepo sherehekeo lingine kubwa katika kusherekea kwa msisitizo mkubwa zaidi ambao bado unatazamiwa katika sura ya kiabishara zaidi na sio kufurahia tu.

Comments

comments

You may also like ...