Header

Kun Aguero apata ajari mbaya ya Gari, avunjika Mbavu

Mshambuliaji wa Klabu ya Soka ya Manchester City pamoja na timu ya Taifa ya Argentina Sergio Kun Aguero amepata ajari ya gari  usiku wa jana akiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege nchini Uholanzi ambako alikuwa amehudhuria tamasha la muziki.

Kwa mujibu wa ripoti Aguero, 29 amevunjika mbavu na atakuwa nje ya uwanja kwa takribani Miezi miwili na atakosa Mchezo dhidi ya Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini England klabu ya Soka ya Chelsea utakaopigwa Jumamosi hii.

Picha zilizosambaa katika baadhi ya Mitandao kutoka nchini Ulolanzi zimeonyesha gari ndogo ambayo Aguero alikuwepo na dereva wake ikiwa imegonga nguzo kati kati ya jiji la Amstedam huku ikiripotiwa kuwa hakuna aliyepoteza Maisha zaidi ya kuumia.

Awali Aguero aliweka picha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa instagram ikimuonyesha yeye na Msanii kutoka Uholanzi anayefahamika kwa jina la Maluma ambaye ndiye aliyemualika staa uyo wa Argentina katika tamasha.

 

Comments

comments

You may also like ...