Header

Sholo Mwamba: Young Dee na Dogo Janja wanagombana sababu ya Muna Love

Staa wa Singeli, Sholo Mwamba, amesema kisa na mkasa cha Young Dee na Dogo Janja kutupiana matusi ya nguoni kwenye interviews ni mrembo aitwaye Muna Love.

Mwamba ambaye amesema alikuwa chini ya usimamizi wa Muna Love kama bosi wake, ameiambia E-News ya EATV kuwa mara nyingi alikuwa akiwakuta rappers hao aliowaita ‘ving’asiti’ miguu juu kwenye makochi kwa bosi wake wakisubiri kuhudumiwa.

Amedai kuwa kilichokuwa kinamuuma ni kuhangaika kufanya show mikoani kisha kumpa bosi wake Muna ambaye naye huwapa rappers hao kwa kazi yao ya ‘mjini msingi kiuno.’

Siku za hivi karibuni, Young Dee na Janjaro wamekuwa wakirushiana matusi ya nguoni. Dee alimuita Janjaro ms*nge na huku rapper huyo wa Arusha akijibu kwa kumuita Dee ni teja.

Comments

comments

You may also like ...