Header

Bale kuiona Wales kwenye Luninga Michezo ya kufuzu Kombe la Dunia

Mshambuliaji wa Klabu ya Real Madrid Gareth Bale ameondolewa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Wales kinachojiandaa na Michezo ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Georgia pamoja na Jamuhuri ya Ireland kufuatia kusumbuliwa na Majeraha eneo la chini ya paja (Calf Strain).

Bale, 28 alikosa Mchezo wa Jumapili kati ya Klabu yake dhidi ya Espanyol ambao Real Madrid waliibuka na ushindi wa Magoli 2-0 kufuatia kusumbuliwa na Majeraha hayo aliyopata kwenye Mchezo wa UEFA Champions dhidi ya Borussia Dortmund.

Awali Bale alijumuishwa kwenye kikosi cha Wales siku ya Jumatatu huku akishindwa kufanya mazoezi ya pamoja na kikosi hicho kabla ya Benchi la ufundi kuamua kumrejesha Madrid.

Wales ipo nafasi ya pili kwenye Kundi D wakizidiwa alama nne na Vinara wa kundi hilo timu ya Taifa ya Serbia huku ikiwa imesalia Michezo miwili tu.

Comments

comments

You may also like ...