Header

Abdu Kiba ataja kilichosababisha ukimya wake

Abdul Kiba ametoa ufafanuzi kuhusu ukimya wake wa muda mrefu kwenye muziki.

Kiba ameiambia Dizzim Online kuwa kitu kikubwa kilichomfanya kukaa kimya ni process za kusaini kwenye lebo ya Kings Music inayomilikiwa na kaka ake Alikiba.

“Sasa hivi nimesajiliwa kwenye lebo mpya ambayo imekuwa ikifuatilia  msanii ambaye anaimba vizuri na kutunga vizuri  na anaweza kumantain  vitu vingi kwenye game,” amesema.

“Pia kuniandaa vizuri ili niweze kurudi kwenye game vizuri kama tunavyojua sasa hivi muziki umekuwa mkubwa sana, so hatuwezi kukurupuka,” amefafanua.

Miongoni mwa nyimbo za Abdu Kiba zilizowahi kufanya vizuri ni Ayaya aliyomshirikisha Ruby.

Comments

comments

You may also like ...