Header

Idris Sultan: Timing ya utani wangu kwa Diamond imeniponza, ila sikumlenga Hamisa!

Mtangazaji wa redio, muigizaji na mchekeshaji, Idris Sultan, ameiambia Dizzim Online kuwa hafikirii kupunguza kitu chochote kwenye kazi yake ya uchekeshaji baada ya jana kuandika utani uliopokelewa vibaya na Hamisa Mobetto.

“Hamna cha kupunguza ni timing tu,” amesema Idris Sultan. “The joke was okay, but nadhani  ilikuwa too soon kwake na kuguswa ingawaje haikulenga katika namna aliyoichukulia yeye Hamisa,” ameongeza.

Kwenye post yake, Idris alimtania Diamond kuwa atampa shilingi 500 ili anunue kondomu kumsaidia kuepukana na kutoa matumizi ya elfu 70 na Rav 4 kwa wanawake anaowazalisha.

Diamond hajasema chochote kuhusu utani huo.

Comments

comments

You may also like ...