Header

licha ya mbwembwe za usajili EPL zaidi ya Paundi Milioni 60 zinatumikia Benchi

Wakati wa Dirisha la Usajili  Ligi kuu nchini England Vilabu mbalimbali vilionyesha jeuri ya pesa kwa kuhakikisha wanasajili wachezaji wanaowataka huku tukishuhudia ada kubwa zikitolewa kwa baadhi ya Wachezaji hasa kwa Vilabu viwili vya Manchester United pamoja na Manchester City bila kusahau Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo Klabu ya Soka ya Chelsea.

Katika Usajili huo baadhi ya Wachezaji waliosajiliwa wameonyesha thamani zao Lukaku ambaye alisajiliwa kwa ada ya Paundi zaidi ya Milioni 75 akitokea Everton na mpaka sasa ndiye kinara wa Ligi hiyo kwa Magoli akiwa na Jumla ya Magoli 7, Morata, Lacazette Nemanja Matic, Bakayoko ni moja wa nyota waliong’ara ambao wamesajiliwa Msimu huu.

Licha ya Wachezaji hao kuna orodha pia ya Wachezaji ambao wamesajiliwa na Vilabu mbalimbali kwa fedha kubwa lakini Mpaka sasa hawajaonekana kucheza katika Ligi hiyo licha ya kuwa na matarajio makubwa hasa kiwango viwango walivyonavyo.

VIctor Lindelof

Moja kati ya Mabeki waliosajiliwa katika Klabu ya Manchester United Msimu huu akitokea katika Klabu ya Benfica ya nchini Ureno kwa ada ya Paundi Milioni 31 huku Mashabiki pamoja na wadau mbalimbali wa michezo walitajiria kumuona Mchezaji huyo akipewa nafasi ndani ya kikosi hicho ukizingatia umri wake wa miaka 23 pamoja na uwezo alio nao hususani ukizingatia kariba ya Mabeki anaowataka Jose Mourinho.

Mpaka sasa Beki huyo hajacheza Mchezo wowote ndani ya Ligi kuu nchini England, ameonekana katika Mchezo wa Ufunguzi wa Michuano ya UEFA dhidi ya Real Madrid lakini pia ameonekana kwenye Mchezo wa Kombe la Carabao Cup ambao United ni Mabingwa watetezi huku akipata nafasi katika Michuano ya UEFA Champions baada ya Eric Bailly pamoja na Phil Jones kutumikia adhabu ya kufungiwa. Mourinho alieleza kuwa Sababu za Mchezaji huyo kutocheza ni kutokana na kutozoea Ligi hiyo na anahitaji muda ili kuzoea na kuendana nayo.

Danny Drinkwater

Danny ni mmoja kati ya Viungo bora wa kati katika Ligi kuu nchini England, ameisaidia klabu ya Leicester City kutwaa Ubingwa wa England kwa mara ya kwanza katika Historia ya Klabu hiyo. Alisajiliwa na Mabingwa watetezi Chelsea siku ya mwisho ya dirisha la usajili huku Mashabiki wa Chelsea wakiamini kuwa Muunganiko wa Kante na Drinkwater ungeweza kuleta matunda kama ilivyokuwa Leicester wakati Wachezaji hao wakicheza pamoja.

Tangu ajiunge na Chelsea hajacheza Mechi yoyote ya Ligi huku akiwa anasumbuliwa na Majeraha huku akitarajiwa kupona baada ya Mechi za kufuzu kucheza kombe la Dunia mwaka 2018 zinazopigwa wiki hii.

Willy Cabarelo, Juan Foyth, Aleksandar Dragovic ni baadhi ya Wachezaji ambao wamesajiliwa na Vilabu mbalimbali nchini England ambao mpaka sasa hajatumikia Vilabu vyao. Kwa Hesabu za haraka haraka kuna zaidi ya Paundi Milioni 60 ambazo zipo benchi mpaka sasa.

 

 

Comments

comments

You may also like ...