Header

Malipo makubwa ya Katy Perry kama jaji wa American Idol yaleta utata

Malipo ya dola milioni 25 aliyopewa Katy Perry kuwa jaji wa shindano la American Idol, yamesababisha rabsha kubwa kwa kituo cha runinga cha ABC kilichoyarudisha.

Kwa mujibu wa tovuti ya Page Six, kiasi hicho kikubwa kwa Perry kimesababisha majaji wengine, Lionel Richie na Luke Bryan walipwe kiduchu. Pia mshahara kwa host wa show hiyo Ryan Seacrest wa dola milioni 15 nao umekatwa kutokana na bajeti.

Chanzo kimedai kuwa ABC ilikuwa imetenga dola milioni 50 kwaajili ya kuwalipa majaji na host lakini imewalazimu kuongeza bajeti kwaajili ya Lionel. ABC kupitia CEO na Rais wake, Ben Sherwood alilazimika kumpa kiasi hicho kikubwa Perry kwasababu anapendwa na watazamaji vijana na ana followers wengi kwenye mitandao ya kijamii.

Bryan na Richie nao walitegemea kupata kiwango sawa na Katy lakini wameishia kupewa kiduchu. Chanzo kimesema walipewa ofa ya dola milioni 2.5 wakakataa na sasa wanapewa dola milioni 7 kila mmoja.

Comments

comments

You may also like ...