Header

‘Mpe Habari Remix’ Stereo aikamilisha na Stamina, BillNass, Jay Moe na kufunga na Khaligraph Jones

Staa wa ngoma ya ‘Mpe Habari’ iliyomshirikisha Rich Mavoko, James Joseph Masanilo a.k.a ‘Stereo’ amekamilisha na kuiachia rasmi kolabo ya ngoma ‘Mpe habari Remix’ ambayo imewashirikisha wachanaji wenye nafasi ya kutambulika kwenye kiwanda cha muziki Tanzania na mkali Khaligraph Jones kutoka Kenya.

Kupitia mtadao wa kuuza muziki Tanzania ‘Wasafi Dot Com(www.wasafi.com’ jana wimbo huo umeingia rasmi kwa lengo la mashabiki kuendelea kujipatia ambapo ngoma hiyo imewadondosha Bill Bass, Jay Moe na Stamina.

Stamina katika utengenezaji wa Mpe ‘Habari Remix’ naye alizungumzia hisia za kufanya kazi na lebo ya muziki ya WCB Wasafi kwa mara ya kwanza.

Haya yalikuwa ni maneno ya awali katika utengenezaji wa Mpe Habri Remix na Dizzim Online alizungumza Mengi na Stereo.

Comments

comments

You may also like ...