Header

Y Tony ashindilia nyingine ya pili chini ya ‘Moja Moja Empire’

Staa wa ngoma ya ‘Mama’ iliyomshirikisha Mkali wa sauti kutoka katika tasnia ya kiwanda cha muziki Tanzania ‘Bongo Fleva’ Barnaba, Heri Michael a.k.a Y Tony ameachia kazi yake nyingine mpya kwa jina la ‘Kibenten’ chini ya uongozi wake wa lebo ya muziki ya ‘Moja Moja Empire’.

Ikiwa ni kazi ya pili chini ya usimamizi wa lebo hiyo inayomilikiwa na mtayarishaji wa muziki ‘Zest Pro’ ambaye ndiye mtayarishaji mkuu wa ngoma hiyo mpya ikiwa ameshirikishana na mtayarishaji mwenza ‘Ruge’ kwa upande wa ukamilishaji na uwekaji sawa sauti zote za wimbo katika ubora mzuri wa kukubalika(Mastered).

Video ya ngoma  hii mpya ya ‘Kibenten’ imeongozwa na ‘Director Manrizo huku wadau na mashabiki wanaofatilia muziki mzuri wameshakutana na Y Tony katika uboora wake wa ngoma kali kama vile KIVULI na TUKAJICHANE.

Comments

comments

You may also like ...