Header

Devvon Terrell awakatisha keki ya wimbo mashabiki wake

Muimbaji, rapa na mkali wa Cover za nyimbo kubwa Duniani na zinazofanya vizuri kutoka lebo ya muziki ya Caroline Records, Devvon Terrell ameachia ngoma iliyohisiwa kuwa zawadi katika tarehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake inayokwenda kwa jina ‘Temperature’.

Mkali huyu ambaye ameshaonekana kuzifanyia Cover ngoma kubwa kisha zikafanya vizuri hasa mitandaoni ameshiriki kuongoza video ya wimbo wake wa ‘Temperature’ huku audio ikikamilishwa kwa ushirikiano wa watayarishaji, David Cappa, Tyler Rohn na Aphillyated.

Hata hivyo Devvon Terrell ambaye ni mzaliwa wa Brooklyn, kumbukumbu zinasema kuwa amezaliwa siku ya 6 ya mwezi Octoba ambayo siku ya jana alitimiza umri wa miaka 29.

Msikilize alichokifanya Devvon Terrell kama Cover ya wimbo wa Rapa Kendrick Lamar ‘Humble’ unaopatikana katikaAlbum yake Kendrick ‘DAMN’ ilitoka rasmi mwaka huu.

Comments

comments

You may also like ...